Wajue kupe wanaoifyonza na kuiua sekta ya elimu nchini

Ni kweli elimu ya bure katika shule za umma inafaa kuwa bure lakini sio hivyo kwa sababu walafi wameifanya iwe ghali.

Wanaosema husema, elimu ni taa inayonga’aa kwenye giza ila kauli hii huenda ni ndoto tu katika nchi yetu ya Kenya hasa kwa wanaotoka familia maskini.

Habari Nyingine: Jalang'o alimlipia karo mwanafunzi aliyefika shuleni na sabuni

Kinachonifanya kusema hivi ni kwa sababu licha ya serikali kila mara kusisitiza elimu ni ya bure wazazi bado wanalipia, na bila shaka utakubaliana nami wengi hawawezi kumudu. Hali zao kiuchumi ni mbovu.

Sio siri tena na ni wazi zipo shule za msingi zinazomilikiwa na serikali ambazo huwatoza wazazi karo sawa na shule za binafsi. Sasa hii ndio elimu bila malipo au bure? Je, hawa wakuu wa shule wanaowalazimisha wazazi kulipa ada baadhi zisizojulikana hufanya hivyo kwa maagizo ya nani? Je, serikali ina habari kuhusu hizi ada au inalifumbia jicho suala hili?

Habari Nyingine: Picha za mwanafunzi aliyewasili shuleni akiwa na sabuni tu ndani ya kasha zawasikitisha Wakenya

Katika shule nyingi za umma hasa za sekondari, wazazi hulazimika kulipa ada nyingi fiche ambazo wengi wanasema hawajui ni za nini. Hulazimika kulipa sababu lisilobudi hubidi ati.

Habari Nyingine: Babu Owino amlipia karo jamaa aliyewacha shule na kuwa bawabu

Kwa mfano zipo shule mpaka sasa wanafunzi wanapojiunga nazo, wazazi hupewa maagizo watakapokwenda kununua sare, vitabu au vifaa wanavyohitajika kuwa navyo kabla ya kusajiliwa. Katika maduka hayo, wazazi hupata bei ni mara dufu hata zaidi ya bei ya kawaida.

Imebainika kuwa, mengi ya maduka hayo na biasara za aina hii ni za walimu wakuu au marafiki zao na hulenga kuwanyonya kama sio kuwafyonza wazazi. Hatimaye kuifanya elimu ya bure kuwa kauli tu.

Habari Nyingine: Wasamaria wema wamsaidia mvulana aliyetembea kutoka Nandi hadi Kakamega kujiunga na sekondari

Wiki hii tumehuhudia visa vingi vya wazazi na watoto wao hasa kutoka familia maskini wakionyesha nyuso za huruma mwingi wakati wakiwapeleka watoto wao shuleni. Ingawa ni wachache wanaopata misaada inayofaa kuwaweka shuleni wengi mtakabali wao haujulikani.

Lakini ni kwa nini nchi iliyohuru kuwaruhusu matapeli na walafi kuwahangaisha wazazi maskini na wanao ambao ndio 'viongozi' wa kesho. Ni kwa nini walimu wakuu wenye tabia za aina hawafutwi kazi?

Habari Nyingine: Bintiye DP Ruto ajiunga na shule ya upili ya Alliance Girls

Swali hili linahitaji kujibiwa na wahusika wakuu katika sekta ya elimu. Wizara pia inafaa kuhakikisha walimu wote wakuu wanafuata utaratibu uliowekwa na sio kutumia njia za kijanja kuwatapeli wazazi maskini.

Vilevile ni wakati serikali itumie vitendo badala ya kauli tupu. Walimu wanaohusika na kuwahangaisha wazazi ni lazima kufunguliwa kesi na kufungwa jela wakipatikana na hatia.

Kama taifa tunahitaji kuiga mifano ya mataifa yaliyopiga hatua katika masuala ya elimu ambayo yameruhusu upatikanaji wa elimu bora bila ya mahangaiko. Tukiiga mfano huo basi tutakuwa tumejali maslahi ya wote. Elimu kwa wote awe maskini au tajiri.

Makala haya yameandikwa na Sakwa Titus mwalimu na mwandishi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaIB0fJJmrpqmkaS2p63NsphmnZyeurZ5yq6ummWXna6ttYyzmKKcmWK7pLTIp6BmpplixKK4yKasZq%2BRoMK2ecyaq5qolaG2brrAZq6anpGjxqKuyJqqoZmilnqtrcahmKJmmKm6rQ%3D%3D