Kocha wa zamani wa Gor Mahia Hassan Oktay apona virusi vya corona

- Hassan Oktay aligunduliwa kuwa na virusi vya corona baada ya kuanza kuugua huku akiwa likizoni Uingereza

- Mkufunzi huyo kwa sasa amepona huku akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumrejeshea afya yake

- Aliongoza Gor Mahia kwa msimu mmoja pekee na kuwasaidia kutwaa ubingwa nyumbani na ushindi katika robo- fainali ya Kombe la CAF

Kocha wa zamani wa Gor Mahia, Hassan Oktay amesimulia namna alikabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Oktay aligunduliwa hii majuzi kuwa na COVID-19 na kumpelekea kulazwa katika hospitali moja jijini London ambapo amekuwa akipokea matibabu.

Habari Nyingine: Chelsea: Mlinda lango nguli wa zamani Peter Bonetti aaga dunia akiwa na miaka 78

Habari Nyingine: Mkenya Michael Olunga ashirikiana na Ligi ya Uhispania kupigana na COVID-19

Lakini baada ya siku 18 ya kupambana na ugonjwa huo hatari, mkufunzi huyo amefichua kwamba amepona huku akishikilia kuwa ni miujiza kuwa hai.

"Hali hiyo ilikuwa mbaya zaidi, nilikuwa na matatizo ya kifua ambayo yalidorora kutokana na virusi vya corona," Oktay aliambia Goal.

"Nilikuwa nimechukua likizo kutoka kwa mchezo na nilikuwa Uingereza ambapo nilianza kuugua. Ni miujizia kuwa hai. Nilikuwa na virusi hivyo mwilini kwa siku 18 na ilikuwa vigumu, Hata hivyo namshukuru Mungu, mambo yamebadilika sasa na niko buheri wa afya," aliongezea Oktay.

Habari Nyingine: Kocha wa zamani wa Gormahia, Hassan Oktay akanusha madai anaugua coronavirus

Kocha huyo mwenye miaka 47, pia alichukua muda kuwatumia wafuasi wake Wakenya ujumbe wa tahadhari dhidi ya ugonjwa huo akiwahimiza kufuata maagizo yaliyowekwa.

"Kile ningependa ni kuwatakia kila mmoja afya njema na kufuata maagizo yaliyotolewa ili kuzuia kuambukizwa ugonjwa huo," alisema kocha huyo.

Oktay aligura K'Ogalo mnamo Agosti 2019, katika hali tatanishi kwa kile alitaja kama sababu za kibinafsi.

Alijunga na klabu hicho mnamo Disemba mwaka 2018, akichukua usukani kutoka kwa Dylan Kerr ambaye pia alitengana na mabingwa hao wa KPL .

Wakati wake Gor, alishinda taji la ligi na kuwasaidia kufikia mkondo wa timu nane bora katika mashindano ya Kombe la CAF.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdjan5zf5RmoqibmJZ6uK2Ms5immZ6eeritjKCmq2WdlrWqrYyhmKyrkaN6sLfTmrBmmaCku6J51aKprquZYsO6rYycpqunnpZ7qcDMpQ%3D%3D